Msimu uliopita wakati wa dirisha dogo la usajili Yanga ilimsajili beki Fiston Kayembe Kanku kutoka nchini DR Congo klabu ya SM Sanga.
Hata hivyo Kayembe alishindwa kuitumikia Yanga na baadae mabingwa hao wa kihistoria kuamua kuachana nae baada ya klabu ya SM Sanga kumuwekea ngumu ikimtuhumu kuvunja mkataba wake kiholela.
Jambo hilo huenda likamkuta mshambuliaji mpya wa Azam Fc Obrey Chirwa ambaye kuna taarifa kuwa timu ya Nogoom El Mustakabal aliyokuwa amesajiliwa nchini Misri imepanga kumburuza CAF baada ya kuvunja mkataba kiholela.
Uongozi wa Azam Fc umekiri kutopata kibali cha Chirwa hivyo hawataweza kumtumia kwenye ligi hadi hapo mgogoro huo utakapisuluhishwa.
Chirwa ilikuwa karibu asajiliwe na Yanga kabla kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kumuwekea ngumu akimtuhumu kuwa mtovu wa nidhamu

ADVERTISE HERE