Zahera achukizwa na waamuzi leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2018
Zahera achukizwa na waamuzi leo
Licha ya Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar leo, kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amelitaka shirikisho la soka nchini (TFF) kuhakikisha linatumia waamuzi wenye uwezo wa kutafsiri ipasavyo sheria za soka kama wanataka kulisaidia soka la Tanzania liweze kuendelea

Zahera amesema timu zote zinazoshiriki ligi kuu ni nzuri lakini kuna tatizo kubwa la waamuzi.

Amesema timu yake leo ni kama ilicheza dhidi ya watu 14 uwanjani kutokana na maamuzi yasiyoridhisha yaliyokuwa yakitolewa na waamuzi.

Katika hatua nyingine Zahera amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi leo licha ya kutopata mda wa kupumzika baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc.

"Nilikuwa na wasiwasi kuwa hali ya uchovu kwa wachezaji wangu ingetuletea matatizo lakini nawapongeza wamepambana mpaka kuibuka na ushindi"

"Sisi tumecheza siku tatu zilizopita lakini wenzetu hawakuwa na mchezo wowote kwa zaidi ya wiki mbili hivyo nawapongeza wachezaji wangu, wamejituma sana leo kwani haikuwa rahisi," amesema
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’