Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amezuia usajili wa wachezaji wapya hadi pale madai ya wachezaji wanaoendelea kuitumikia Yanga sasa yatatuliwe, imefahamika.
Kocha huyo ambaye amejipambanua kwa kuwa muwazi katika utaratibu wake wa kufanya kazi, amesema ana orodha ya wachezaji 10 ambao wana madai kutokana na mikataba yao walioingia na Yanga na anaona ni vyema wachezaji hao wakapewa kipaumbele kwa kutatua madai yao kabla ya kuleta wachezaji wapya.
"Hatuwezi kusajili wachezaji wapya wakati bado tungali na wachezaji ambao wanamadai, ni vyema tukamalizana nao kwanza," amesema.
"Ni sawa umeshindwa kumlipia ada ya shule mtoto wako uliyenae nyumbani halafu unachukua na mtoto wa kaka yako ili umsomeshe!"
Zahera amesema Yanga inakabiliwa na changamoto ambazo ni vyema zikatatuliwa kabla ya kufikiri mambo makubwa zaidi.
Amesema matokeo mazuri wanayopata sasa yanatokana na juhudi binafsi za wachezaji na benchi la ufundi pamoja na viongozi wa Yanga.
Lakini msimu huu timu hiyo ni kama inacheza bila ya kuwa na malengo.
Amesema alipotua Yanga hakupewa malengo yoyote iwapo kama ni kuchukua ubingwa au kumaliza nafasi ya pili au kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao
Amesema hali hiyo ilisababishwa na hali ya kiuchumi ya klabu hiyo kwa sasa.

ADVERTISE HERE