Mkutano wa Baraza Kuu la Bodi ya Ligi (TPLB) unatarajia kufanyika kesho Jumamosi Disemba 1,2018 Jijini Tanga.
Mkutano huo utafanyika kwenye hotel ya Regal Naivera saa 3 asubuhi.
Aidha Mkutano huo utatumika kujaza nafasi zilizo wazi za Mwenyekiti na Mjumbe anayewakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza na Mjumbe anayewakilisha klabu za Ligi Daraja la Pili.
Steven Mnguto ndiye mgombea pekee anayegombea nafasi ya Mwenyekiti wakati Azim Khan na Brown Ernest wakigombea nafasi ya Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Kwanza na Michael Kadebe yeye akigombea nafasi ya kuwakilisha klabu Ligi Daraja la Pili.
Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi inajazwa baada ya TFF kumuondoa aliyekuwa Mwenyekiti wake Clement Sanga kufuatia maamuzi ya Wanachama wa Yanga kumtambua Yusufu Manji kuwa Mwenyekiti halali wa klabu hiyo hivyo kumfanya Sanga aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo kukosa sifa.
Hata hivyo TFF sasa ni kama inaupinga uamuzi wake huo wa awali kwani inaendelea na mchakato wa kusimamia uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Januari 13 2019.
Uchaguzi huo pia utahusisha nafasi za Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa kamati ya Utendaji

ADVERTISE HERE