Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kujikusanyia alama 35 kutoka michezo 13.
Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema wachezaji wa Yanga wanastahili pongezi kwa mafanikio wanayopata hasa katika kipindi hiki ambacho Yanga inapita
"Wachezaji wamekuwa wakijituma sana, wanastahili pongezi kwa mafanikio haya. Sasa tunaongoza ligi, ni wachache sana waliofikiria kama Yanga itaweza kuwa nafasi hii," amesema Zahera
βTutapambana kuhakikisha tunaendelea kubaki kileleni. Nataka wachezaji wangu wajitume zaidi kwenye kila mchezo kuhakikisha tunaendeleza rekodi yetu ya kutopoteza mchezo wowote, kila mchezo mmoja tunapomaliza tunajipanga kwa mchezo mwingine,β alisema Zahera.
Yanga licha ya kupitia katika kipindi kigumu nje na ndani ya uwanja, bado imeenedelea kufanya vizuri ambapo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi hiyo.

ADVERTISE HERE