Juzi wakati akihojiwa na waandishi wa habari baada ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Prisons dhidi ya Yanga, Mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akitokwa na machozi.
Zahera amesema hali ya upambanaji iliyoonyeshwa wachezaji wake mpaka kupelekea kuibuka na ushindi mnono licha ya mazingira magumu waliyokabiliana nayo, ilimfanya alie
Amesema wachezaji wake wanakabiliwa na hali ngumu, wengi wakicheza kwa kujitolea hivyo maamuzi ya uonevu waliyofanyiwa kwenye mchezo huo yalimuumiza sana
"Mungu alikuwa upande wetu kwani mazingira wanayopita wachezaji wangu hawakustahili kufanyiwa uonevu ule na waamuzi," amesema Zahera
Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons umeifanya Yanga ijikite kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha alama 38
Azam Fc imeendelea kubaki nafasi ya pili licha ya hapo jana kuilaza Stand United mabao 3-1 na kufikisha alama 36 ikiwa imecheza michezo 14 sawa na Yanga
Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 27, ambazo ni alama 11 nyuma ya vinara wa ligi Yanga

ADVERTISE HERE