TFF yaomba radhi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2017
TFF yaomba radhi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeomba radhi kwa wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jana Jioni.

Hayo yameelezwa na taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa Shirikisho hilo, Alfred Lucas na kusema Ngao iliyotolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu ya Simba dhidi ya Yanga katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penati 5-4 na kutwaa ngao hiyo.

"Watanzania hususani wanafamilia wa mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri muonekano wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika", alisema Alfred.

Pamoja na hayo, Alfred amesema wameshawasiliana na uongozi wa Simba SC ili waweze kuirudisha Ngao hiyo iweze kufanyiwa marekebisho yatayobaki kwenye kumbukumbu sahihi.

Kwa upande mwingine, Shirikisho hilo limesema halitegemei tukio kama hilo kujitokeza kwa mara nyingine.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’