Zahera awaita matajiri wainusuru Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
6 Dec 2018
Zahera awaita matajiri wainusuru Yanga
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewashangaa matajiri wenye mapenzi na klabu hiyo kwa kushindwa kuisaidia timu hiyo ambayo kwa sasa imekumbwa na ukata.

Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha pointi 38 katika mechi 14 walizocheza, lakini taarifa ndani ya klabu hizo zinadai timu imekumbwa na ukata na kushindwa kulipa wachezaji mishahara kwa zaidi ya miezi mitatu.

Zahera ameeleza kushangazwa na timu hiyo kuishi kimasikini wakati ina wanachama ambao ni matajiri.

Kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alikwenda mbali zaidi na kusema licha ya wanachama hao kushindwa kuisaidia timu hiyo, anashangaa wanaopiga hela kwa mgongo wa timu hiyo.

“Timu haina hela hilo lipo wazi, nawashangaa matajiri wenye mapenzi na hii timu wapo wapi, wao ndio wanaweza kuisaidia timu kutoka hapa ilipo," Zahera amenukuliwa na gazeti la Bingwa

“Si kwamba timu haiingizi hela, hapana, kuna wajanja wachache wanaendelea kuing’ang’ania timu mikoani, wanagombania ukuu wa msafara na kupiga hela ndefu ambazo zingeweza kutusaidia kulipana mishahara,” alisema.

Zahera alisisitiza kuwa kilichomleta Yanga si fedha bali ni kufundisha soka ikiwa ndiyo kazi yake, lakini pia kuendelea kuboresha wasifu (CV) wake, akiamini lazima ataipaisha Yanga.

“Nilipotua nakumbuka niliambiwa maneno mengi sana kuwa Yanga haina fedha hivyo ningetaabika sana, lakini hilo halinisumbui mimi kwa sababu nataka kuona Yanga inafanya vizuri,” alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →