Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Biashara United utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.
Zahera amesema wachezaji Ibrahim Ajib na Mrisho Ngasa hawatakuwa sehemu ya mchezo huo wakati Heritier Makambo ana asilimia 50 za kucheza baada ya kupata majeraha mazoezini leo
Aidha Kelvin Yondani, Papi Tshishimbi na Gadiel Michael wamepona majeraha yao na Mcongoman huyo amesema watakuwa sehemu ya mchezo huo.
Zahera amesema anatambua mchezo wa kesho utakuwa mgumu kutokana na nafasi iliyopo klabu ya Biashara United
"Tumejiandaa vyema kuwakabili Biashara maana mara zote unapocheza na hizi timu ndogo ambazo ziko chini kwenye msimamo huwa zinakamia sana lakini tumejiandaa kikamilifu kuwakabili," amesema Zahera

ADVERTISE HERE