TFF yataja wagombea waliopitishwa kuwania uongozi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Dec 2018
TFF yataja wagombea waliopitishwa kuwania uongozi Yanga
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza majina yaliyopitishwa kwenye usaili wa Wagombea Uongozi wa Klabu ya Young Africans.

Usaili umefanyika kwa siku 3 Alhamis Novemba 6,2018,Ijumaa Novemba 7,2018 na Jumamosi Novemba 8,2018 Makao Makuu ya TFF Karume,Ilala.

Nafasi ya mwenyekiti Wagombea waliochukuwa na kurudisha fomu walikuwa 3,Wagombea waliopitishwa ni wawili Baraka Igangula na Jonas Tiboroha wakati mgombea Erick Minga ameenguliwa kufuatia taarifa zake alizojaza kwenye fomu kutofautiana na nyaraka halisi.

Nafasi ya Makamu mwenyekiti wagombea waliopitishwa ni 3 Titus Osoro, Pindu Luhoyo na Salum Magege Chota wakati Mgombea mmoja Yoni Kevela ameenguliwa kwa matakwa ya kikatiba baada ya kuchukuwa fomu kugombea nafasi mbili kwa wakati mmoja Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.

Nafasi ya Ujumbe waliopitishwa ni Athanas Kazighe,Ramadhan Said,Salim Rupia,Dominic Francis,Shafii Amri,Benjamin Mwakasonda,Christopher Kashiririka,Ally Msigwa,Silvester Haule,Arafat Haji,Frank Kalokole na Said Kambi.

Wagombea Wanne wameshindwa kufika kwenye usaili Hamad Islam,Seko Kongo,Leonard Marango na Benard Mabula kwa mujibu wa kanuni wameenguliwa katika uchaguzi.

Wagombea ambao hawajapitishwa wanayo haki ya kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’