FT : Yanga 2-1 Biashara United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Dec 2018
FT : Yanga 2-1 Biashara United
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga wameendeleza ubabe kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuilaza Biashara United mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa leo.

Huo ulikuwa ushindi wa 13 kwa Yanga katika michezo 15 waliyocheza, wakitoka sare michezo miwili tu

Biashara United iliandika bao la kuongoza kwenye dakika ya 38 baada ya kufanya shambulizi la kushitukiza lililomaliziwa vyema na Mangalo



Yanga imedhihirisha kuwa ni timu isiyofungika kwa urahisi kwani katika kipindi cha pili ilipeleka mashambulizi mengi langoni kwa Biashara United waliokuwa wakicheza kwa kujihami

Bao la kusawazisha la Yanga liliwekwa kambani na Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye kwenye mchezo wa leo kocha Mwinyi Zahera alimchezesha kama kiungo



Shaibu alimalizia vyema pasi murua ya Amisi Tambwe aliyeingia katika kipindi cha pili.

Aliyeipa Yanga matokeo muhimu sio mwingine zaidi ya Heritier Makambo aliyefunga bao safi kwenye dakika ya 80 na kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu

Makambo aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliopita, amefikisha mabao nane sasa akiwa nyuma ya Eliud Ambokile wa Mbeya City kwa tofaurti ya bao moja tu.

Makambo alifunga bao jingine kwenye dakika za majeruhi lakini mwamuzi alilikataa akidai kuwa aliushika mpira kabla ya kuutumbukiza kimiani

Yanga imerudi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 41, alama mbili zaidi ya Azam Fc iliyo nafasi ya pili

Aidha matokeo hayo yanaifanya Yanga izidi kuitimulia vumbi Simba sasa ikiachwa kwa tofauti ya alama 14 licha ya kuwa na michezo mitatu ya kiporo
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’