Zahera kufanya maamuzi magumu michuano ya kombe la Mapinduzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Dec 2018
Zahera kufanya maamuzi magumu michuano ya kombe la Mapinduzi
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameliomba Shirikisho la soka nchini (TFF) kusogeza mbele mchezo wa ligi kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga uliopangwa kupigwa Disemba 29 ili wachezaji wapate muda wa kupumzika kabla ya kwenda kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza mwishoni mwa mwezi huu.

Zahera amesema kama mabadiliko hayo hayatafanyika basi atalazimika kupeleka visiwani Zanzibar kikosi cha pili cha Yanga cha wachezaji wa umri chini ya miaka 20 kushiriki michuano hiyo.

Licha ya uwepo wa michuano ya Mapinduzi Cup, mwezi ujao pia kutakuwa na michuano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Januari 22 mpaka Januari 27 2019.

Michuano ya kombe la Mapinduzi itaanza mwishoni mwa mwezi huu na itafikia tamati Januari 12 2019.

Zahera amehofia michuano hiyo inaweza kuathiri mwenendo wa timu yake kwenye ligi kama wachezaji hawatapata muda wa kutosha wa kupumzika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
53m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’