Zahera alivyogoma wachezaji wake kugawanywa na Beno

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Dec 2018
Zahera alivyogoma wachezaji wake kugawanywa na Beno
Uamuzi wa kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera kugoma kumpokea kikosini mlinda lango namba moja wa timu hiyo Beno Kakolanya umeshangaza wengi.

Jana mmoja wa wadau wa Yanga Cyprian Musiba alijitolea kulilipa deni la Mil 15 ambalo Kakolanya anaidai Yanga ikiwa ni sehemu ya fedha zake za usajili

Musiba alimkabidhi Kakolanya fedha taslim Tsh Mil 2 na kuahidi kuzilipa fedha zilizobaki kwa makubaliano maalum.

Hata hivyo tukio hilo linatajwa kumuharibia zaidi Kakolanya ambaye alijiondoa katika kikosi cha Yanga kwa karibu mwezi mzima akisubiri alipwe fedha zake

Zahera aligoma kumpokea Kakolanya na kuwataka wale waliomshawishi asihudhurie mazoezi ya Yanga wamtafutie timu kabla dirisha la usajili halijafungwa baadae leo.

Mcongomani huyo alibainisha kuwa ana wachezaji 10 ambao pia wanadai fedha zao za usajili lakini hawakugoma, wameendelea kutimiza majukumu yao katika kikosi cha Yanga.

Iwapo atamruhusu Kakolanya arudi kikosini baada ya kulipiwa fedha zake, atakuwa amehalalisha njia iliyotumiwa na mlinda lango huyo kutumiwa na wachezaji wengine kudai stahiki zao

"Waliomshawishi Beno kwa pesa je wataweza kuwalipa na wachezaji wengine iwapo watagoma wakidai stahiki zao?," alihoji Zahera

"Utaratibu huu siutaki sababu unaweza kuigawa timu yangu. Kwa kuwa mwenyewe (Beno) aliandika barua ya kusitisha mkataba wake basi mimi siko tayari kumpokea"

"Ni vyema akajiunga na timu itakayomfaa. Muda bado upo kwa kuwa dirisha la usajili litafungwa saa sita usiku"

Zahera amebainisha kuwa Kakolanya alikuwa akidai fedha za usajili pekee hakuwa na madeni ya mishahara

Amesema mlinda lango huyo hakufukuzwa na Yanga, bali alijiondoa yeye mwenyewe iwe kwa utashi wake au kwa kushawishiwa.

Uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa umekuwa ukilipa na utaendelea kulipa madeni ya wachezaji wake ingawa malipo hayo yanafanyika kwa awamu kutokana na changamoto za kifedha zilizoikumba klabu hiyo kwa sasa
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’