FT : Yanga 3-2 Ruvu Shooting

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Dec 2018
FT : Yanga 3-2 Ruvu Shooting
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga wameendeleza ubabe leo baada ya kuilaza Ruvu Shooting mabao 3-2 katika mchezo mkali uliopigwa uwanja wa Taifa.

Bao la dakika za lala salama lililowekwa kambani na Heritier Makambo 'Makambovic' limeihakikishia Yanga alama tatu muhimu zilizoiimarisha kileleni baada ya kufikisha alama 44.



Yanga ilianza kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 11 kupitia kwa Amisi Tambwe baada ya mpira murua wa Ibrahim Ajib kutua mguuni kwa Makambo aliyemramba chenga mlinda lango wa Ruvu Shooting kabla mpira haujakutana na mguu wa Tambwe.

Ruvu Shooting walionyesha upinzani mkali kwa Yanga leo na walifanikiwa kusawazisha bao kwenye dakika ya 31 kupitia kwa Fully Maganga.

Timu zilikwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.

Katika kipindi cha pili timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini Yanga ilicharuka zaidi katika dakika 15 za mwisho na ilifanikiwa kufunga bao la pili kupitia kwa Feisal Salum 'Fei Toto' aliyefunga bao safi la kideoni katika dakika ya 78

Fei Toto alikutana na mpira nje kidogo ya 18 na kufumua shuti kali lililojaa kwenye nyavu za juu kulia langoni kwa Ruvu Shooting.

Ruvu Shooting walisawazisha tena kwenye dakika ya 84 kwa bao la mkwaju wa penati la Said Dilunga kabla Ajib hajamtengenezea Makambo kuifungia Yanga bao la ushindi kwenye dakika ya 94.

Ushindi huo umeiimarisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 44, alama nne mbele ya Azam Fc.

Yanga imezidi kuitimulia vumbi Simba ambayo sasa itahitaji kukusanya alama 17 kuwafikia mabingwa hao wa kihistoria.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’