Zahera amkana kipa mpya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Dec 2018
Zahera amkana kipa mpya Yanga
Ukiachilia mbali lawama alizotoa kwa viongozi kwa kushindwa kusajili wachezaji aliowataka, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemkana mlinda lango aliyesajiliwa na timu hiyo Ibrahim Hamid kuwa hamfahamu.

Zahera amesema amepewa taarifa leo juu ya kusajiliwa kwa mlinda lango huyo.

"Mimi huyu kipa mpya simjui. Nimeshangaa viongozi wamesajili bila kunitaarifu," Zahera amewaambia waandishi wa habari leo.

Kuhusu msimamo wake kwa mlinda lango Beno Kakolanya Zahera amesema ana makubaliano na wachezaji wote kuhusu migomo ya kudai maslahi yao.

"Tulikubaliana kuwa kama mchezaji anaona hawezi kucheza kwa kuwa hajalipwa ajiondoe kabisa kwenye timu na sio kugoma kuja mazoezini"

"Mimi sipendi mchezaji ambaye leo anakuja mazoezini kesho haji sababu anadai pesa yake. Kama wachezaji wote watafanya hivyo tutaharibu kazi," amesema

"Makambo hakulipwa tangu ametua nchini, walizuia vitu vyake hotelini juzi ndio wamelipa deni la hoteli lakini hakuwahi kugoma. Ni kwa sababu anajua kocha alisema ukigoma anakufukuza"

Aidha Zahera amebainisha kitendo cha Kakolanya kulipwa Mil 2 na mdau wa Yanga Cyprian Musiba nusura kiharibu utulivu ndani ya kikosi chake.

"Walinifuata wachezaji wawili, Andrew Vicent na Juma Abdul kuniuliza kuwa wameona mwenzao amelipwa lakini wao mbona hawalipwi?"

"Anayetaka kuwalipia wachezaji madeni basi ni vyema akawasiliana na viongozi wa Yanga ili kuwalipia wote wanaodai"

Zahera amesisitiza hayuko tayari kumpokea Kakolanya.

"Nimewaambia viongozi wa Yanga siku wakimrudisha Kakolanya kwenye timu basi nitaondoka mimi"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
46m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’