Zahera anachochea kasi ya Yanga - Yondani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2018
Zahera anachochea kasi ya Yanga - Yondani
Yanga imeanza vyema msimu kwa kufanikiwa kushinda michezo 14 na kutoka sare miwili ikiwa imeshuka dimbani mara 16.

Inaongoza ligi baada ya kujikusanyia alama 44.

Ni Yanga na Azam Fc pekee ambazo hazijapoteza mchezo mpaka sasa msimu huu.

Hata hivyo Yanga inakabiliwa na changamoto za kiuchumi hali ambayo mwanzoni mwa msimu ilionekana kama ingeigharimu timu hiyo

Lakini mambo yamekuwa tofauti, mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa yamewashangaza wengi.

Nahodha wa mabingwa hao wa kihistoria Kelvin Yondani ametaja mambo matatu ambayo yameifanya Yanga iwe hapo ilipo licha ya kukabiliwa na 'ukata'

Kwanza Yondani amemsifia kocha wa timu hiyo Mcongomani Mwinyi Zahera kuwa mbinu zake zimeweza kuisaidia timu hiyo iweze kufanya vizuri.

Lakini pia Yondani amesema Zahera amekuwa kama mzazi kwao.

Amekuwa akiwajenga wachezaji kisaikolojia na kuwafanya wajihisi wanadeni kubwa la kuhakikisha Yanga inapata matokeo kila inaposhuka dimbani

Jambo jingine ambalo nahodha huyo amelibainisha ni wachezaji kujitambua.

Yondani amesema licha ya kukabiliwa na hali ngumu, wameamua kujitoa ili kuhakikisha hawaharibu mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.

Yondani amesema mpira ni kazi yao na wameona ni vyema waendelee kutimiza wajibu wao kwani wanaamini madai na mahitaji yao yatamalizwa.

Kesho Alhamisi Yanga itashuka kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kuikabili African Lyon katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
39m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’