Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga leo wanashuka kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kuikabili African Lyon katika mchezo wa kiporo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Yanga iko mkoani Arusha tangu juzi Jumanne, ikifanya maandalizi kuelekea mchezo huo.
Vinara hao wa ligi kuu leo wanashuka dimbani bila ya kuwa na kocha wao Mkuu Mwinyi Zahera ambaye alisafiri kwenda Ufaransa kushughulikia masuala yake ya biashara.
Zahera atarudi Jumatano ijayo, Disemba 26 2018.
Yanga pia itawakosa baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi na wengine wanatumikia adhabu ya kadi
Thaban Kamusoko, Raphael Daudi na Andrew Vicent wameongeza orodha ya majeruhi wakiungana na Juma Mahadhi na Baruani Akilimali
Feisal Salum atakosekana kwenye mchezo wa leo akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Mrisho Ngasa pia atakuwa anamalizia adhabu yake ya kadi nyekundu akikosa mchezo wa tatu
Mcongomani Papi Tshishimbi yeye alifiwa na baba mkwe wake na alisafiri kurejea Congo kuhudhuria msiba huo
Hata hivyo kikosi cha Yanga kimejipambanua kwa kufanya vizuri bila ya kumtegemea mchezaji mmoja mmoja.
Msimu huu Yanga imecheza michezo mingi na ikaweza kupata matokeo pasipo kuwa na wachezaji wake waandamizi
Ushindi katika mchezo wa leo utaweza kuikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama saba dhidi ya Azam Fc iliyo nafasi ya pili

ADVERTISE HERE