Walinzi wa kati wa Yanga Kelvin Yondani, Andrew Vicent na Abdallah Shaibu 'Ninja' wamefunga mabao manne na kuifanya safu ya ulinzi ya Yanga kuwa na rekodi ya kipekee.
Wakati Yondani na Chikupe wakiwa wamefunga bao moja moja, Shaibu ametupia mabao mawili.
Kwenye mchezo uliopita dhidi ya African Lyon Shaibu angeweza kufunga mabao zaidi ya mawili kama angekuwa na utulivu.
Mfumo wa kushambulia na kujilinda kwa pamoja 'toto football' unaotumiwa na Kocha Mwinyi Zahera umekuwa ukiwanufaisha walinzi hao ambapo wamekuwa wakisogea mbele kuongeza mashambulizi hasa katika mipira ya adhabu na kona
Kiwango cha Ninja kimekuwa kikiimarika siku hadi siku ambapo kocha Zahera pia ameanza kumtumia kama kiungo kwenye baadhi ya michezo baada ya kubaini ana uwezo wa kucheza namba zaidi ya moja.
Ninja anatajwa kuwa mrithi halisi wa mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alistaafu mwanzoni mwa msimu huu na kukabidhiwa wadhifa wa Umeneja wa vinara hao wa ligi kuu