Licha ya mashabiki wengi bila ya kujali timu zao kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuiunga mkono Mtibwa Sugar katika mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya KCCA, timu hiyo imeondoshwa katika michuano hiyo baada leo kufungwa mabao 2-1 na hivyo kufungwa jumla ya mabao 5-1.
Kukosa uzoefu katika michuano hiyo inatajwa kuwa sababu iliyoigharimu Mtibwa Sugar kufungashiwa virago kwa kipigo cha aibu.
Msimu uliopita Yanga ilitinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ikifanya hivyo mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Yanga imepania kurejea anga za Kimataifa msimu ujao ambapo vinara hao wa ligi kuu wanapaswa kutwaa taji moja kati ya ligi kuu au ASFC
Keshokutwa Jumatatu Disemba 24 Yanga itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya ASFC kuikabili Tukuyu Stars katika mchezo utakaopigwa dimba la Taifa.
Matokeo ya ASFC, michezo ya leo