Licha ya kuwa ameanza mazoezi mepesi, mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe huenda ataukosa mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Lipuli kesho Jumapili.
Tambwe anasumbuliwa na maumivu ya goti. Alipata majeraha hayo siku moja kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na alishindwa kucheza kwenye mchezo huo.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu, amethibitisha kuumia kwa Tambwe na amesema atarudi uwanjani baada ya wiki moja.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema wanaamini katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara huenda watamtumia straika huyo.
Baada ya mchezo huo na Lipuli, mabingwa watetezi klabu ya Yanga watasafiri kwenda mikoa ya kusini ambapo wikiendi ijayo watacheza na Njombe Mji na baadaye Majimaji.
Sasa Yanga itawakosa wachezaji watano katika mchezo wake wa Jumapili ambao ni Obrey Chirwa, Beno Kakolanya, Geofrey Mwashiuya, Burhani Yahya na Amissi Tambwe.
Pius Buswita nae amefungiwa mwaka mmoja na TFF akidaiwa kusaini katika timu mbili, Simba na Yanga.

ADVERTISE HERE