Zahera kutua leo akitokea Ufaransa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2018
Zahera kutua leo akitokea Ufaransa

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwasili nchini leo akitokea Ufaransa alikokwenda wiki iliyopita kushughulikia masuala binafsi ya kibiashara.

Taarifa zilizopatikana mapema leo zimebainisha Zahera atatua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa nane mchana.

Kuondoka kwake wiki iliyopita kuliibua hofu miongoni mwa mashabiki wa Yanga wakiamini huenda kocha huyo alikuwa 'amesepa' moja kwa moja kukimbia changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga.

Hata hivyo akiwa Ufaransa Zahera aliwahakikishia WanaYanga kuwa atarudi na kusisitiza hakufuata maslahi kwenye klabu ya Yanga.

Kulithibitisha hilo juzi aliwataka mashabiki wa Yanga kuichangia timu ili iweze kusafiri kwenda Mbeya kwa usafiri wa Ndege mwenyewe pia akiahidi kuchangia pesa ya ziada kama kutakuwa na upungufu.

Zahera pia amekuwa akitoa pesa zake kuwapa wachezaji wanapofanya vizuri

Ni kocha ambaye kwa sasa amejipambanua kuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga kutokana  na kujitoa kwake katika kipindi hiki ambacho Yanga inapitia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’