Sio ajabu mashabiki kuichangia Yanga - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2018
Sio ajabu mashabiki kuichangia Yanga - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga amesema sio jambo la ajabu kwa mashabiki kuisaidia timu yao na amewashangaa wanaohoji kuhusu utaratibu huo unaotumiwa na Yanga.

Juzi akiwa nchini Ufaransa Zahera aliwataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuichangia timu ili iweze kwenda mkoani Mbeya kwa usafiri wa Ndege. Na hatimaye leo timu imefanikiwa kwenda Mbeya kwa usafiri huo.

"Ni jambo la kawaida sana kwa mashabiki kuisaidia timu yao," amesema Zahera

"Timu kama Real Madrid, FC Barcelona zinaingiza pesa nyingi sana kwa utaratibu huo. Labda ni hapa Tanzania tu ambapo huo utaratibu bado haujazoeleka"

"Wale mashabiki wenye mapenzi ya kweli na timu zao wanakuwa tayari kuzisaidia. Sasa sisi kuwaomba mashabiki wetu kuichangangia timu kuna jambo gani la ajabu? "

Zahera amewashukuru mashabiki waliochangia timu na kufanikisha safari ya mkoani Mbeya akiahidi wao watalipa fadhila hiyo kwa kuhakikisha timu inapata ushindi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’