FT : Yanga 1-1 Lipuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2017
FT : Yanga 1-1 Lipuli
Mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi timu iliyopanda daraja msimu uliopita, Lipuli FC, umemalizika kwa sare ya bao 1-1.

Ikicheza kwa kujihami kwa muda mwingi Lipuli ilianza kuhesabu bao kwenye dakika ya 44, Seif Abdallah akiifungia bao hilo baada ya walinzi wa kati wa Yanga kuzembea.

Donald Ngoma aliisawazishia Yanga bao kwenye dakika ya 45. Akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Juma Abdul.

Kipindi cha pili Lipuli ilipaki basi, na kuifanya Yanga itawale karibu dakika zote za kipindi hicho.

Licha ya Yanga kutawala kipindi chote cha pili ilikosa mbinu ya kutumbukiza mpira wavuni.

Donald Ngoma alikaribia kuifungia Yanga bao la pili kwenye dakika ya 78 baada ya kupokea pasi murua ya Raphael Daudi lakini alichelewa kufanya maamuzi hivyo mlinda lango akaokoa hatari langoni mwake.

Kamusoko aliyekuwa akin'gara katikati ya dimba alipata nafasi kadhaa za kufunga lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Lipuli uliwezesha timu hiyo inusurike na kipigo.

Aidha Lipuli ilitumia mbinu ya kupoteza muda kwenye kipindi cha pili baada ya kuzidiwa na mashambulizi.

Mwamuzi aliongeza dakika nne za ziada licha ya ukweli kwamba Lipuli ilipoteza muda mwingi zaidi ya huo

Ni dhahri Mwalimu Lwandamina anahitaji kuifanyie kazi safu ya ushambuliaji.

Aidha Yanga bado inawakosa wachezaji wake muhimu Amissi Tambwe, Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa kutokana na kuwa majeruhi.

Tambwe na Mwashiuya huenda wakawa tayari kucheza mchezo dhidi ya Njombe Mji wakati Chirwa anasubiri hatma yake baada ya shirikisho la soka nchini TFF kusema ana kesi ya kujibu kufuatia tukio la kumsukuma mwamuzi kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC msimu uliopita.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’