Mwigulu atambia usajili wa Fei Toto Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Dec 2018
Mwigulu atambia usajili wa Fei Toto Yanga

Mdau mkubwa wa klabu ya Yanga Mwigulu Nchemba amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuichangia Yanga kwa kuwa ni timu yao (timu ya Wananchi).

Licha ya kuwa Rais wa Singida United, Mwigulu huwa hafichi U-Yanga wake ambapo amefichua kuwa hata usajili wa Feisal Salum 'Fei Toto' aliukamilisha yeye mahsusi kwa ajili ya Yanga kama mchango wake kwa klabu hiyo.

"Fei Toto hakusajiliwa na Singida United hivyo hakuwa mchezaji wetu," Mwigulu aliwaambia wanaandishi wa habari waliohoji kwa nini mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka JKU alitolewa Singida United na kupelekwa Yanga.

"Nilimsajili kutoka JKU kwa ajili ya kumpeleka Yanga. Wakati ule tulikuwa tumapambania kwa kuwa Yanga ilikuwa bado haijaamua wachezaji inaotaka kuwasajili. "

Fei Toto ni miongoni mwa wachezaji bora kabisa waliosajiliwa na Yanga mwezi Juni 2018. Amekuwa moja ya 'engine' za Yanga zilizoifanya timu hiyo mpaka sasa iwe haijapoteza mchezo kwenye ligi.

Mabao yake mawili aliyofunga kwenye ligi, ni miongoni mwa mabao bora kabisa yaliyofungwa mpaka sasa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’