Tusikatishwe tamaa na sare ya bao 1-1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2017
Tusikatishwe tamaa na sare ya bao 1-1
Kila mmoja alitegemea leo Yanga ingepata ushindi dhidi ya Lipuli katika mchezo wa kwanza wa VPL msimu huu.

Sare ya bao 1-1 ni moja ya matokeo ya mchezo na matokeo hayo hayana maana kuwa Yanga haitaweza kufanya vizuri msimu huu.

Bado naamini Yanga ina kikosi kipana cha kuweza kutetea ubingwa wake. Kilichotokea leo ni moja ya matokeo ya mchezo tu.



Yanga ina wachezaji wengi majeruhi naamini wakirejea itarudi kwenye kiwango chake.

Ni Juzi tu kwa wale wanaofuatilia ligi kuu ya Uingereza tulishuhudia mabingwa watetezi Chelsea FC wakichapwa mabao 3-2 na Burnley tena kwenye dimba lao la nyumbani.

Hivyo tusikate tamaa na kuanza kushusha lawama kwa viongozi, kocha na hata wachezaji eti kwa kuwa wameshindwa kupata ushindi.

Ndio, timu ikipoteza au hata kutoa sare wakati mwingine inauma sana kwa mashabiki, lakini hayo ndio matokeo ya mchezo.

Tuwe bega kwa bega na timu yetu inaposhinda, inapofungwa na pale inapotoka sare. Tutakuwa mashabiki wa ajabu sana kama tutaisapoti timu pale inaposhinda tu na kuitelekeza pale inapofungwa au kutoka sare.

Tuwe na Yanga wakati wote. Kwanza timu hii ndiyo timu yenye mafanikio kuliko nyingine yeyote nchini Tanzania. Tumefanikiwa kutwaa taji la VPL kwa msimu mitatu mfululizo, sio jambo dogo.

Sasa hivi michezo yote ya Yanga itakuwa kama fainali kwa kuwa kila timu itataka ipate ushindi dhidi ya mabingwa wa kihistoria.

Tumeshuhudia jinsi wachezaji walivyojituma hasa kwenye kipindi cha pili. Walikosa bahati tu ya kuutumbukiza mpira wavuni lakini mashambulizi yalikuwa mengi.

Dakika 20 za mwisho wachezaji wote wa Lipuli walirudi langoni kwao kuzuia. Wachezaji kumi kuwa nyuma ya mpira inahitaji ubunifu wa hali ya juu kuweza kufunga.

Naamini mwalimu ameona na atayafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza. Tunachoweza kufanya sisi tulio nje ni kuwapa ushauri viongozi na benchi la ufundi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’