Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi kikiwa kimesheheni wachezaji wengi kutoka kikosi cha pili cha Yanga.
Idadi kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza wanabaki jijini Dar es salaam wakiendelea na mazoezi kujiandaa na michezo ya ligi, kombe la FA na SportPesa Super Cup.
Mkakati wa kocha Mwinyi Zahera ni kuhakikisha Yanga inamaliza mzunguuko wa kwanza bila ya kupoteza mchezo, ukiwa umebaki mchezo mmoja dhidi ya Azam Fc ambao uliahirishwa ili kupisha Mapinduzi Cup.
Mchezo dhidi ya Azam huenda ukapigwa baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Mapinduzi.
Hata hivyo Yanga na Azam Fc zitakutana huko Zanzibar katika mchezo wa kombe la Mapinduzi utakaopigwa Januari 05 2019.
ADVERTISE HERE