Mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili amesema wananufaika na uwepo wa kocha Mwinyi Zahera katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria.
Kabwili amesema Zahera anafanya kazi zaidi ya moja katika kikosi cha Yanga.
"Licha ya kuwa Mwalimu wetu, Zahera ni kama mzazi kwetu, " amesema Kabwili
"Ni mshauri na mtu anayependa kuona kila mchezaji anafanikiwa. Yuko karibu sana na wachezaji"
"Kwangu binafsi nimefundisha na makocha wengi lakini naona Zahera yuko tofauti sana, ndiye kocha bora zaidi kwangu"
Akizungumzia malengo ya kikosi chao msimu huu Kabwili amesema baada ya kumaliza mzunguuko wa kwanza wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, sasa wanataka kuhakikisha wanatwaa ubingwa.
"Lengo letu kuu sasa ni kutwaa ubingwa. Moto tuliomaliza nao mzunguuko wa kwanza tutauendeleza katika mzunguuko wa pili"
Yanga imejihakikishia kukamilisha mzunguuko wa kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 50.
Matokeo yoyote katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Azam Fc hayawezi kuwaondoa kileleni.
Aidha vinara hao wa ligi ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi mpaka sasa, ikiwa imeshinda michezo 16 na kutoka sare michezo miwili