Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemteua kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib kuwa nahodha wa timu.
Ajib amechukua nafasi ya Kelvin Yondani ambaye Zahera amemvua madaraka hayo baada ya leo kushindwa kuhudhuria mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichobaki jijini Dar es salaam bila ya kutoa sababu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga mapema leo, wachezaji waliobaki jijini Dar es salaam wameanza mazoezi ya utimamu wa mwili pia kwa upande wa uwanjani kulikuwa na mafunzo maalumu juu ya umakni uwanjani(Concentration) pamoja na umaliziaji kwenye safu ya Ushambuliaji.
Mazoezi ya leo yalikwa chini ya kocha Mkuu Mwinyi Zahera.
Ikumbukwe msaidizi wake Noel Mwandila yeye na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi wapo Zanzibar wakiwa na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza pamoja na wale wa kikosi cha U20 kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi.