Yanga yaiwinda Azam Fc Zanzibar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2019
Yanga yaiwinda Azam Fc Zanzibar

Baada ya hapo jana kuilaza KVZ kwa bao 1-0 na kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi B kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga leo wamejifua visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc.

Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Januari 05 kwenye uwanja wa Amaan.

Yanga imedhihirisha kuwa na kikosi kipana kwani wachezaji wengine ambao hawakusafiri kwenda Zanzibar nao wamejifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na michezo ya ligi.

Licha ya kuwa na kikosi kilichosheheni wachezaji wengi kutoka timu ya vijana ya Yanga, Kocha Msaidizi wa timu hiyo Noel Mwandila amesema hawaihofii Azam Fc na wako tayari kupambana nayo kesho

Katika mchezo wake wa kwanza, Azam fc iliyowajumuisha washambuliaji wa zamani wa Yanga Donald Ngoma na Obrey Chirwa huku kikosi chake kikiwa na wachezaji nane wa kigeni,  ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Jamhuri.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’