Igangula aahidi kuharakisha mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2019
Igangula aahidi kuharakisha mabadiliko Yanga

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Yanga wamezindua rasmi kampeni za kujinadi yale yote ambayo wamepanga kuyafanya kama wakipata nafasi za kuiongoza klabu hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika leo ukiongozwa na Mbaraka Hussein Igangula kwenye Ukumbi wa Wallace Kata ya 15 CCM uliopo Temeke jijini Dar es Salaam.

Igangula ni mgombea nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo ambayo Mei 20 mwaka juzi alijiuzulu mfanyabiashara maarufu nchini Yussuf Manji.

Akizinduzi kampeni hizo, Igangula alisema lengo lake ni kutaka kuhakikisha klabu hiyo inahamia kwenye mfumo wa soka la kisasa ili wawe na nguvu kubwa ya kiuendeshaji.

"Ndani ya mwaka wangu mmoja nitafanya mabadiliko makubwa ikiwemo maboresho ya jengo letu, pamoja na kuhakikisha Yanga inakuwa na uwanja wake wa kufanyia mazoezi.

"Mfumo wa uwekezaji utarahisisha mambo ndani ya klabu yetu,  lengo ni kutaka Yanga iwe na nguvu kubwa, pia nitakuwa makini na vyanzo vyetu vyote vya mapato, " alisema.

Igangula amekuja na kauli mbiu isemayo Umoja na mshikamano kwa maendeleo ya Yanga

Mgombea huyo yupo sambamba na makamu wake Titus Ossoro pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji, Silvester Bernard Haule, Benjamini Mwakasonda, Atanas Kazige, Ramadhan Said (Chalinze).

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’