Baada ya malalamiko ya muda mrefu hatimaye uongozi wa Yanga umetangaza kusaka Mzabuni wa kusimamia mauzo ya jezi za klabu hiyo.
Msimu huu Yanga imetoa matoleo mengi ya jezi hali iliyopelekea kuwachanganya mashabiki wa timu hiyo kushindwa kufahamu zipi ni jezi rasmi za Yanga na ni wapi pa kuzipata
Jana Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Siza Lyimo ambaye pia ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo alisema wametangaza zabuni .
"Tumetangaza zabuni ya mauzo ya jezi ili wanayanga waweze kununua jezi halisi za klabu," amesema
"Ni kweli hatukuzindua jezi kama walivyofanya wenzetu hii imewachanganya wanayanga kushindwa kutambua jezi rasmi za klabu hivyo kupitia mzabuni atakayepatikana itaondoa hii sintofahamu na watanunua jezi rasmi"
Msimu huu klabu ya Yanga imetoa zaidi ya matoleo sita ya jezi huku jezi hizo zikionekana kutengenezwa na kampuni tofauti tofauti