Kamusoko asisitiza haondoki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2019
Kamusoko asisitiza haondoki Yanga

Kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko amefafanua juu ya ujumbe wake alioandika kwenye mitandao ya kijamii siku chache zilizopita ambao amesema ulieleweka vibaya kwa baadhi ya wadau wa klabu ya Yanga.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Kamusoko amefafanua kuwa ujumbe huo ulikuwa kwa ajili ya kuwashukuru Wana Yanga kwa kuendelea kumuunga mkono tangu alipotua katika klabu hiyo misimu minne iliyopita

"Habari za jioni kwa mashabiki wangu na wale wote wanaonipenda. Napenda kuchukua nafasi hii ili kueleza vizuri kuhusu post yangu ya juzi kwasababu naona watu wengine wamechukulia tofauti na wameiweka vibaya," ameandika Kamusoko

"Mimi nimeweka hiyo post kushukuru tu upendo kutoka kwenu mashabiki na watu wote wa Yanga sio kwamba eti nilimaanisha kua naondoka hapana"

"Mimi nimeona ni post ili watu waone kua na appreciate upendo ambao munanipa sio kwamba naondoka kwenye timu nadhani nimeliweka sawa. Asanteni sana," amefafanua Kamusoko

Huenda ujumbe huo ulieleweka vibaya kutokana na ukweli kwamba mkataba wa Kamusoko na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu na bado hakuna uhakika kama mkongwe huyo ataongeza mktaba mwingine kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’