Kiungo ambaye ni habari ya mjini kwa mashabiki wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, ameangalia ukuta wa timu hiyo akawaambia viongozi anawaletea bonge la beki fundi, kulingana na gazeti la Mwanaspoti.
Tshishimbi, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyenunuliwa na Yanga akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland, amewahakikishia mabosi wa Yanga kuwa kama beki huyo akitua na kushirikiana vizuri na waliopo, hao mastraika wanaoogopwa akina Emmanuel Okwi hawatafua dafu.
Habari za uhakika ni kwamba mchezaji huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuona aina ya uchezaji wa timu za Simba na Lipuli walizovaana nazo.
Yanga inahaha kusaka beki wa kati wa kuziba nafasi ya Mtogo Vincent Bossou aliyemaliza mkataba, baada ya kushindwa kufanya usajili mpya dakika za mwishoni kutokana na kubanwa na kanuni za Ligi Kuu Bara.
Yanga inahitaji kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kusajili mchezaji mwenye kiwango cha juu ili kuweza kufanya vizuri kwenye ligi na muhimu zaidi kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika ambapo msimu huu imetoa kipaumbele zaidi kwa michuano hiyo.

ADVERTISE HERE