Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imemruhusu beki wa Yanga Andrew Vicent Chikupe aitumikie timu hiyo baada ya kumkosa na hatia.
Chikupe alipelekwa katika Kamati hiyo akituhumiwa kumpiga kichwa mwamuzi wa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Prisons dhidi ya Yanga uliopigwa Disemba 03, 2018.
Chikupe alisimamishwa kuitumikia Yanga akisubiri maamuzi ya Kamati hiyo ambayo hata hivyo imesema ushahidi uliowasilishwa haukutosha kumtia hatiani.
Chikupe amekosa michezo minne na sasa yuko huru kuitumikia Yanga kesho kwenye mchezo dhidi ya Mwadui Fc
Beki huyo kisiki pia amepona majeraha ya goti yaliyokuwa yakimsumbua
ADVERTISE HERE