FT : Yanga 3-1 Mwadui Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jan 2019
FT : Yanga 3-1 Mwadui Fc

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wameendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuilaza Mwadui Fc mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa leo Jumanne jioni.

Huo ulikuwa ushindi wa 17 kwa Yanga katika michezo 19 iliyocheza mpaka sasa ikitoka sare michezo miwili na kufikisha alama 53

Yanga imedhihirisha ni timu isiyotegemea mchezaji mmoja katika kuzifumania nyavu kwani katika mchezo wa leo haikuwa na kinara wake wa mabao Heritier Makambo

Aliyenza kuifungia Yanga bao la kuongoza ni nahodha mpya wa timu hiyo Ibrahim Ajib aliyefunga bao kwenye dakika ya 12 kwa mpira wa adhabu akiwa umbali wa karibu mita 30

Katika dakika ya 18 Ajib angeweza kuiongezea Yanga bao la pili kama mkwaju wake wa penati usingedakwa na mlinda lango wa Mwadui Fc.

Hata hivyo Ajib alisahihisha makosa yake kwenye dakika ya 39 baada ya majaro yake kutua kichwani kwa Amissi Tambwe aliyeiandikia Yanga bao la pili

Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Vijana hao wa Mwinyi Zahera walirejea na kasi waliyomaliza nayo kipindi cha kwanza na walifanikiwa kuandika bao la tatu kwenye dakika ya 58 kupitia kwa Feisal Salum 'Fei Toto'

Ni bao jingine lililofungwa kwa ustadi mkubwa na Fei Toto akiachia fataki akiwa nje ya 18. Sasa imekuwa ni tabia kwa Toto kufunga mabao ya aina hiyo.

Bao la kufutia machozi kwa upande wa Mwadui Fc lilifungwa na Salim Iyee kwenye dakika ya 81

Matokeo hayo yameendelea kuikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi wakifikisha alama 53, alama 13 zaidi ya Azam fc inayoshika nafasi ya pili

Yanga sasa imeizidi Simba alama 20!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’