Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hakuna mchezaji ambaye atakosekana katika kikosi cha Yanga atamfanya akose usingizi kwa kuwa timu yake haitegemei mchezaji mmoja.
Zahera amesema kikosi chake kwa sasa kimekamilika na kinaweza kufanya vizuri kwa kutumia wachezaji wanaokuwepo
"Hakuna mchezaji hata mmoja ambaye naweza kusema akikosekana timu itashindwa kufanya vizuri, hakuna mchezaji anaweza kunifanya nikashindwa kulala kwa sababu ya kukosekana kwenye kikosi," amesema Zahera
"Tumeshacheza mechi tano bila Ajibu tukashinda zote, Yondani hakuwepo mechi saba tukashinda zote, Makambo hakuwepo mechi mbili tukashinda zote."
Zahera ameiongoza Yanga kushinda michezo kumi mfululizo, tisa ya ligi na mmoja wa kombe la FA (ASFC)
ADVERTISE HERE