Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wameondoka jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Ndege kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Stand United
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumamosi, Januari 19 2019

Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga mapema leo, kikosi cha wachezaji 18 na viongozi wa benchi la Ufundi 'wamepaa' kwenda Shinyanga
"Msafara wa Kikosi chetu tayari umeondoka mapema leo kuelekea Shinyanga kwa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Stand United utakaochezwa jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage," imesema taarifa ya Yanga
"Msafara una wachezaji 18 pamoja na benchi la ufundi ukiwa na kiongozi wa msafara Kaimu Mwenyekiti ya klabu Samwel Lukumay"


ADVERTISE HERE