Inaelezwa mlinda lango Klaus Kindoki atakwenda Congo kuhani msiba wa Baba yake baadae kutokana na hali ya kisiasa iliyoko nchini humo
Eneo analotoka Klaus ambalo liko pembezoni mwa nchi hiyo linadaiwa kukumbwa na machafuko ya kisiasa yaliyopelekea kuchelewa kuzikwa kwa baba yake
Mlinda lango huyo alipata taarifa ya kifo cha Baba yake mapema tangu wakati kikosi cha Yanga kiko Zanzibar lakini changamoto hiyo ilimfanya ashindwe kusafiri
Maziko ya Mzee Kindoki yatafanyika Jumapili bila uwepo wa Klaus na atakwenda huko kwa ajili ya kuhani msiba huo mzito.
Hivyo Kindoki yupo, na huenda akawa langoni kwenye mchezo wa kesho, uamuzi wa mwisho ukiwa wa kocha Mwinyi Zahera
ADVERTISE HERE