Wapinzani wa Yanga katika robo fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup Kariobangi Sharks wametua nchini jana tayari kwa mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumanne katika uwanja wa Taifa
K Sharks inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Kenya
Yanga inayotarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam leo ikitokea mkoani Shinyanga, imeipa kipaumbele michuano hiyo ambayo bingwa wake atanyakua kombe na kitita cha fedha zinazofikia Mil 70
Pia bingwa wa michuano hiyo atapata nafasi ya kuikabili Everton katika mchezo utakaopigwa mwezi Julai 2019
Timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu ni mabingwa watetezi Gor Mahia, Yanga, Simba, SIngida United, Mbao Fc, Kariobang Sharks, Bandari Fc na AFC Leopards
Baada ya kushiriki misimu miwili bila ya mafanikio huku msimu uliopita ikitolewa kwenye raundi ya kwanza, msimu huu Yanga imepania kusaka ubingwa wa michuano hiyo