Malengo ya ubingwa yako palepale - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2019
Malengo ya ubingwa yako palepale - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akiwataka waendelee kuiunga mkono timu yao ili itimize azma ya kutwaa ubingwa msimu huu

Juzi Yanga ilipoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Stand United, matokeo ambayo yamewasononesha mashabiki wa timu hiyo

Zahera amesema wachezaji wake walipambana kwenye mchezo huo lakini walikosa bahati.

Amesema wataendelea kupambana katika michezo ijao ili kuhakikisha wanatwaa ubingwa

"Haukuwa mchezo mwepesi, wachezaji wangu walipambana, lakini hatukuwa makini kuzitumia nafasi tulizozitengeneza, nawapongeza Stand kwa ushindi," alisema Zahera na kuongeza,

"Kwetu bado mapambano yanaendelea, hatujakatishwa tamaa kupoteza mchezo huu. Tutapambana kutimiza lengo letu la kutwaa ubingwa msimu huu"

Baada ya kumalizika michuano ya SportPesa, Yanga inakabiliwa na michezo mitatu ya ugenini dhidi ya Coastal Union, Singida United na JKT Tanzania kisha kurejea jijini Dar es salaam kuikabili Simba

Michezo hii minne inayofuata itatoa mwanga wa hatma ya ubingwa kwa vinara hao wa ligi wanaoongoza kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya Azam Fc iliyo nafasi ya pili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’