Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hali ya uchovu imechangia kwa kiasi kikubwa timu yake kufungwa na Kariobangi Sharks mabao 3-2 kwenye mchezo wa robo fainali michuano ya SportPesa Cup
Yanga ilipata mapumziko ya siku moja tu ikitokea mkoani Shinganga kuikabili Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara ambao nao uliisha kwa mabingwa hao wa kihistoria kukubali kipigo cha bao 1-0
"Tumepoteza mechi leo kutokana na kuchoka kwa safari ya Shinyanga ilikuwa ngumu. Tulikaa Mwanza masaa saba wachezaji walichoka," amesema Zahera
"Wachezaji wangu wanalaumu waamuzi lakini hawakuwa na makosa, waamuzi walichezesha vizuri"
"Katika kipindi cha kwanza tulifanya makosa mengi, lakini tulicheza vizuri zaidi kwenye kipindi cha pili"
Yanga imeondoshwa katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.
Msimu uliopita michuano hiyo ilipofanyika nchini Kenya Yanga ilifungwa na Kakamega HomeBoyz mabao 3-1