Hivi 'viporo' vya Simba ni lazima vipigiwe kelele

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
23 Jan 2019
Hivi 'viporo' vya Simba ni lazima vipigiwe kelele

Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu imekosa mvuto baada ya TFF kushindwa kuiendesha kwa weledi

Ukiachilia mbali suala la ligi kukosa mdhamini, mkanganyiko wa ratiba unaonekana kuondoa radha ya ligi hiyo

Wakati timu nyingine zikiwa zimecheza michezo 23, mabingwa watetezi Simba wamevunja rekodi kwa kuwa na michezo pungufu wakizidiwa michezo TISA

Sababu inayotolewa na Bodi ya ligi ni timu hiyo kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa, sawa lakini maswali mengi yanaibuka ukitazama wingi wa viporo

Sidhani duniani kama kuna ligi ambayo timu moja inaweza kuwa na idadi kama hiyo ya viporo, yaweza kuwa Tanzania imevunja rekodi

Kuna wakati Simba ilipumzishwa karibu mwezi mzima kucheza michezo yao wakisubiri mechi zao za ligi ya mabingwa

Wengi walihoji 'likizo' hiyo waliyopewa Simba lakini walipuuzwa

Wakati huu ligi ikiwa imeingia mzunguuko wa pili ni vyema timu zote zikawa hazitofautiani michezo mingi. Sana sana isiwe zaidi ya michezo miwili

Msimu uliopita Yanga ilishiriki michuano mitatu kwa wakati mmoja, yaani ligi, kombe la Shirikisho na kombe la FA

Ilikuwa ni kawaida kwa timu hiyo kucheza kila baada ya siku mbili au tatu

Wakati mmoja ilitokea visiwa vya Shelisheli na kuunganisha moja kwa moja mkoani Ruvuma kucheza na Majimaji katika mchezo wa kombe la FA

Ilipotoka Songea ikaelekea moja kwa moja mkoani Mtwara ambako siku mbili baadae ikaumana na Ndanda Fc

Lakini hali imekuwa tofauti kwa Simba msimu huu

Ni hatari sana ligi kuwa na mazingira kama haya kwa timu moja kuwa na michezo mingi mkononi kuliko timu nyingine

Utaratibu huu unatengeneza mazingira ya kupanga matokeo

Mfano kama Simba itaendelea kurundikiwa viporo zaidi, wakati itakapoanza kucheza watakuwa na ufahamu wa matokeo gani wanapaswa kupata ili waweze kujiwekea mazingira ya kutetea ubingwa wao.

Ikumbukwe Simba iko hatarini kutoshiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao kama haitatwaa ubingwa.

Tayari imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA, na hakuna dalili njema kwao kuwa na ubavu wa kutwaa taji la ubingwa wa Afrika

Katika mazingira hayo unaweza ukatumika hata utaratibu usio wa kimichezo ili kuhakikisha lengo la kutetea ubingwa linafanikishwa

Duniani kote waandaaji wa ratiba wanahakikisha kuweka umakini ili kusitokee mazingira ya timu moja kuwa na ushawishi wa kupanga matokeo

Miaka miwili nyuma Simba iliwahi kugoma kuendelea kucheza michezo yao wakishinikiza Azam na Yanga zicheze michezo yao MITATU ya viporo lakini leo yao imefika TISA lakini hata wao wenyewe hawajishangai

Lakini hata viongozi wa timu nyingine ikiwemo Yanga hawahoji mazingira haya wakiamini kuwa timu yao inaweza kushinda michezo yote na kutwaa ubingwa bila ya kujali michezo ya mpinzani wao

Lakini ikitokea Yanga imepoteza mchezo mmoja zaidi au hata kutoka sare, kimahesabu Simba itaweza kuwaondoa kileleni kama watashinda michezo yao yote ya viporo

Ni vyema Yanga nao wakashinikiza TFF na Bodi ya Ligi wavipangie ratiba viporo hivi vya Simba ili kuhakikisha angalau kuanzia raundi ya 30 timu zote zikawe na michezo sawa kuondoa mazingira yoyote yanayoweza kushawishi upangaji wa matokeo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’