Licha ya Azam Fc hapo jana kuibuka na ushindi wa mabo 2-1 dhidi ya Biashara United na kufikisha alama 47, bado wanaendelea kushika nafasi ya pili wakiachwa alama sita na vinara wa ligi Yanga huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 20
Hata kama Yanga itasimamishiwa michezo yake na kuiruhusu Simba icheze michezo sita ili kufikisha 20, Yanga itaendelea kubaki kileleni kwa tofauti ya alama mbili
Baada ya kupata mafanikio makubwa katika michezo ya raundi ya kwanza, mabingwa hao wa kihistoria wana nafasi nzuri ya kurejesha ubingwa Jangwani kama watarudia mafanikio hayo

ADVERTISE HERE