Michuano ya SportPesa Cup imefikia tamati leo kwa Kariobang Sharks kutawazwa mabingwa wa michuano hiyo iliyokuwa ikifanyika katika dimba la Taifa
K. Sharks imetwaa taji hilo baada ya kuwafunga ndugu zao wa Bandari Fc kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali
K. Sharks ndio iliiondoa Yanga hatua ya robo fainali ikipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria
Timu za Kenya zimeendelea kutawala michuano hiyo zikishinda kwa msimu wa tatu mfululizo
Katika mchezo wa mapema wa kusaka mshindi wa tatu Simba ilishinda kwa mikwaju ya penati 5-3 dhidi ya Mbao Fc baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana
K. Sharks imejishindia dola 30,000 na imepata tiketi ya kuchuana na Everton mwezi Julai katika mchezo utakaopigwa nchini Kenya