Zahera asuka upya safu ya ulinzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jan 2019
Zahera asuka upya safu ya ulinzi Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema katika michezo ya hivi karibuni mabeki wa timu hiyo wamekuwa wakifanya makosa ya waziwazi yanayopelekea kufungwa mabao mepesi

Yanga imeruhusu mabao manne katika michezo miwili iliyopita.

Iliruhusu bao moja dhidi ya Stand United na ikaruhusu mabao matatu kwenye mchezo dhidi ya Kariobang Sharks

Zahera amesema anafanyia kazi tatizo hilo ili kuhakikisha walinzi wake wa kati na wale wa pembeni hawafanyi makosa yatakayoigharimu zaidi timu

Licha ya mashabiki kumtupia lawama mlinda lango Klaus Kindoki, Zahera amesisitiza katika michezo miwili iliyopita, mabao iliyofungwa Yanga hayatokani na makosa ya kipa

"Tumekuwa tunafanya makosa makubwa mabeki wa kati na hata wa pembeni wamekuwa wakitusababishia matatizo, Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti

"Tunafanya kazi sasa ya kuondoa kasoro hizo na tutaendelea na kazi hii, makosa kama haya hayatakiwi kutokea mara kwa mara kwa timu inayotaka kuchukua ubingwa."

Yanga inajifua katika uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam ikijiandaa na mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Biashara United utakaopigwa Alhamisi, Januari 31 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’