TFF izisaidie timu zote zinapokuwa na majukumu ya CAF - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jan 2019
TFF izisaidie timu zote zinapokuwa na majukumu ya CAF - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzisaidia timu zote zinapokuwa na majukumu ya michuano ya CAF bila kubagua kwani timu inayofanikiwa inanufaisha Taifa

Zahera ambaye msimu uliopita aliiongoza Yanga kumalizia ratiba ya michezo ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi, amesema msimu huu TFF imetimiza wajibu wake kwa kuisaidia Simba kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano hiyo

Lakini ameshangazwa kuwa hali ilikuwa tofauti kwa timu yake msimu uliopita ambapo ilikabiliwa na ratiba isiyo rafiki licha ya kushiriki michuano hiyo

"Viongozi wa TFF wanapaswa kuziangalia timu zinazocheza mashindano ya CAF na kuzisaidia zote bila kujali ni Simba, Yanga au Mtibwa," Zahera ameuambia mtandao wa ShaffihDauda

"Yanga tulienda kucheza Kenya na Gor Mahia siku mbili baadaye tukatakiwa tukacheze Shinyanga.

"Timu zisifanyiwe hivi ili kuwachosha wachezaji kwa makusudi kwa sababu Yanga ikifanya vizuri nchi inapata pointi nyingi na inaweza kuongezewa timu nyingine badala ya kutoa timu mbili zitakuwa tatu."

"Sisi (DR Congo) tuna timu nne, Zambia wana timu nne kwa sababu gani Tanzania iendelee kubaki na timu mbili? Inabidi kuzisaidia timu zinazocheza mashindano ya CAF."

"Walifanya vizuri kuipumzisha Simba kabla ya kwenda kucheza na Nkana ilikuwa vizuri, wachezaji walipumzika wakapata nguvu wakaenda kupata matokeo ya kufungwa 2-1 ambayo yalikuwa ni mazuri kwao."

"Lakini haifai kuipumzisha Simba halafu ikifika zamu ya Yanga mnawaambia wacheze, mnakuwa mnapoteza wenyewe nafasi ya kuongeza timu kwenye mashindano ya Afrika."

Msimu huu Simba imeweka rekodi ya kuwa na 'viporo' vingi kutokana na ushiriki wao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Timu hiyo mpaka sasa iko nyuma kwa michezo tisa dhidi ya timu nyingine ambazo baadhi zimeshashuka dimbani mara 23 huku yenyewe ikiwa na michezo 14

Idadi hiyo ya michezo itaendelea kuongezeka kwani wakati wakiondoka leo kuelekea nchini Misri kuikabili Al Ahly, mwishoni mwa wiki ligi inatarajiwa kuingia mzunguuko wa 24

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’