Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema wadhamini wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ligi kuu ya Tanzania Bara kampuni ya BikoSports ilipaswa kuingia makubaliano na timu kabla ya kuwatumia wachezaji kutangaza bidhaa zao.
Ten amesema mchezaji ni mali ya klabu hivyo hawezi kutumiwa na kutangaza biashara bila kuwepo makubaliano na timu inayommiliki

"Yanga inadhaminiwa na Sportpesa na siyo BikoSports. Kumvalisha mchezaji Heritier makambo fulana yenye tangazo bila makubaliano au taarifa kwa klabu si jambo sahihi na linaleta mkanganyiko mkubwa," amesema ten
"Bodi ya ligi litizameni hili upya linaweza kutuondolea wadhamini"
"Mchezaji ni mali ya klabu, kwa vyoyote lazima kuwe na maelezo au makubalino pande zote, hasa ukizingatia kampuni hizi zina ushindani kibiashara"