Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera leo alimpumzisha mazoezi ya asubuhi mshambuliaji wa timu hiyo Amissi Tambwe aliyepata majeraha ya kupasuka juu ya jicho kwenye mchezo dhidi ya Biashara United na kupelekea akashonwa nyuzi tano.
Tambwe alipata majeraha hayo baada ya kugongana na mlinda lango wa Biashara United Nurdine Balora ambaye pia alipasuka na kulazimika kufungwa bandeji kichwani kuweza kuendelea na mchezo. Balora alitolewa na kocha Amri Saidi mda mchache baadae.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga mapema leo, Zahera amesema Tambwe atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachosafiri mkoani Tanga kwenda kuikabili Coastal Union Februari 03 kisha kuelekea mkoani Singida kuikabili Singida United, Februari 06
ADVERTISE HERE