FT : Coastal Union 1-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Feb 2019
FT : Coastal Union 1-1 Yanga

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kuondoka na alama moja mkoani Tanga baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa dimba la Mkwakwani

Mchezo huo ulioanza kwa kasi, ulizishuhudia timu zote zikishambuliana kwa zamu katika kipindi cha kwanza huku Yanga ikionekana kuwa hatari zaidi kwenye dakika za mwanzoni mwa kipindi hicho

Coastal Union yenye kawaida ya kutofungika kirahisi inapocheza na Yanga katika dimba lake, ilitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 30 likifungwa na Haji Ugando kwa kichwa

Katika kipindi cha pili ni Yanga iliyokuwa hatari zaidi huku Coastal Union ikishambulia kwa kushitukiza

Mabadiliko ya kocha Mwinyi Zahera kumtoa nahodha Ibrahim Ajib na kumuingiza Deus Kaseke yaliisaidia Yanga kusawazisha bao hilo lililofungwa na Kaseke kwenye dakika ya 76 akimalizia krosi ya Matheo Anthony aliyepokea pasi 'mpenyezo' kutoka kwa Thabani Kamusoko

Coastal Union ilimaliza na wachezaji 10 uwanjani baada ya kiungo wake Mussa Abushehe kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi ya makusudi Gadiel Michael wakati wakiwania mpira

Matokeo hayo yataendelea kuibakisha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama saba dhidi ya Azam Fc baada ya kufikisha alama 54

Aidha katika mchezo huo Yanga ilipata pigo baada ya kiungo wake Feisal Salum kuumia mapema katika kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na mkongwe Haruna Moshi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’