Singida yamlalamikia Gustapha, Yanga yawalalamikia Mwashiuya, Zahir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2019
Singida yamlalamikia Gustapha, Yanga yawalalamikia Mwashiuya, Zahir

Wakati uongozi wa klabu ya Singida United ukidai kinda Gustapha Saimon hakuwa na leseni halali ya kuichezea Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu jana, wachezaji wa Singida United Rajab Zahir na Geofrey Mwashiuya waliofungiwa na TFF mwezi Januari kutokana na makosa mbalimbali, wanalalamikiwa baada ya kucheza mchezo huo huku wakiwa hawajalipa faini walizopaswa kulipa

Zahir na Mwashiuya walifungiwa kukosa michezo mitatu na kulipa faini ya Tsh 500,000/- fedha ambazo imedaiwa hazikulipwa hivyo hawakuwa na sifa ya kucheza mchezo wa jana

Naye Mkurugenzi wa Singida United Festos Sanga amesema wamewasilisha malalamiko TFF wakipinga Yanga kumtumia Gustapha Saimon wakidai ni mchezaji halali wa timu ya daraja la kwanza ya Dar City FC

Hata hivyo Gustapha aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili cha Yanga baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika mwezi Januari 2019 visiwani Zanzibar, ana leseni halali iliyotolewa na TFF

Nayo klabu ya Singida United imeonyesha leseni inayomtambulisha Gustapha kama mchezaji halali wa Dar City FC

Mkurugenzi wa kituo cha kulelea vipaji KISA Academy ambako ndipo alipotoka Gustapha, ametoa ufafanuzi wa kuwa kinda huyo ni mchezaji halali wa Yanga kwa kuwa klabu hiyo ilifuata taratibu zote za kumsajili

Amesema Dar City ilimuomba mchezaji huyo akacheze kwa mkopo na hata baada ya kuuzwa kwenda Yanga TFF ilifuta leseni yake ya awali aliyokuwa akitumia Dar City

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’